Top Ad unit 728 × 90

‘AUNTY EZEKIEL’ AWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE BAADA YA PICHA ZAKE ZA NUSU UCHI KUTANDA KWENYE MITANDAO…!!




MSANII wa filamu bongo ambaye anatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni, Aunty Ezekiel, amewaomba radhi mashabiki wake baada ya picha zake zinazomuonesha umbo lake la ndani kusambaa kwenye mitandao, huku akidai kuwa alipigwa picha hizo akiwa amelewa sana.

Picha za msanii huyo zimechukua sura mpya kwenye mitandao mingi ya kijamii, ambapo picha hizo zinataka kufanana na zile za mwanadada nyota wa video za wasanii wa bongo
Agnes ambazo bado zinapatikana kwenye mitandao hiyo ya kijamii.

Kwa mujibu wa mtandao wa DarTalk baada ya kusamba kwa picha hizo mtandao, ulitaka kujua ni kitu gani kilichosababisha hadi kupigwa kwa picha hizo huku nguo aliyokuwa amevaa ikiwa haina heshima mbele za watu, alidai kuwa haikuwa akili yake kwani alikuwa amelewa kiasi kwamba hakuna alichokuwa anakijua siku hiyo ya tukio mjini
Tanga.

Msanii huyo alidai anaamini tukio hilo limetokea na hana budi kukaa kimya au kujiteteta lakini kikubwa anawaomba radhi wale walioziona picha hizo kwani yenye ni mwanadamu hajakamilika.


“Nimeziona kwa kweli ni picha ambazo zinaonesha umbo langu lakini nachoweza kusema kwa sasa ni kwamba wanaomba msamaha mashabiki wangu wote kwani kilichotokea ni kwa sababu ya pombe na nimejifunza kutokana na makosa,”
alisema Aunty.
‘AUNTY EZEKIEL’ AWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE BAADA YA PICHA ZAKE ZA NUSU UCHI KUTANDA KWENYE MITANDAO…!! Reviewed by Unknown on Thursday, September 13, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.