Top Ad unit 728 × 90

‘AY’ AMTABIRIA MAKUBWA MAZURI ‘OMMY DIMPOZ’…!!

MSANII anayefanya muziki kimataifa huku akiwa tayari ameshafanya na wasanii kibao wa nje, nchi kama USA, Nigeria, Kenya, Uganda na nyingine nyingi, Ambwene Yessaya ‘AY’, amesema kuwa anaamini kati ya wasanii wa bongo ambao wanaweza kufikia kiwango kikubwa kimataifa ni Ommy Dimpoz, kwani kila anapokuwa naye mara nyingi huwa anapenda kujua muziki wa nje unavyokuwa.

AY
aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye televisheni moja, ambapo alitakiwa kumtaja msanii mmoja kwenye game ambaye anaweza kufika katika kiwango cha juu hasa kimataifa ndipo alipomtaja Dimpoz kuwa ana vingezo kadhaa ambavyo amekuwa akiviona kutoka kwake.

Hata hivyo alidai kuwa mara nyingi anapokutana naye amekuwa akiulizwa maswali na Dimpoz kuhusiana na nyanja za biashara ya muziki wa kimataifa.
‘AY’ AMTABIRIA MAKUBWA MAZURI ‘OMMY DIMPOZ’…!! Reviewed by Unknown on Friday, September 28, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.