Top Ad unit 728 × 90

Dayna aanza kuachana na VIMINI!

Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said au maarufu kwa jina la ‘Dayna’, amesema anafanya juhudi kuwapagawisha mashabiki wake kwenye shoo zake bila kutegemea kuvaa vimini na kushindwa kuusitiri mwili wake.
Akizungumza kwa siku tokea mkoani Morogoro, Dayna alisema anafanya mipango ya kuachana na aina hiyo ya mavazi, hasa kwenye shoo, akiwa na lengo la kujiweka tofauti katika kazi zake za muziki.
Alisema mtu anapovaa kimini kifupi, anapokuwa jukwaani anashindwa kujimwaga vizuri kwa kuogopa kuonyesha nyeti zake, hivyo jamii kumshusha thamani kama wanavyodharauliwa baadhi yao.
“Nafanya juhudi kuwaaminisha mashabiki wangu kuwa si lazima nivae nguo fupi ya kubana katika shoo zangu, ukizingatia kwamba naweza kuvaa suruali au hata gauni lenye heshima na mashabiki wakanikubali.
Dayna kwa sasa anatamba na nyimbo mbalimbali, ukiwamo ule wa Nivute Kwako na Fimbo ya Mapenzi.

Dayna aanza kuachana na VIMINI! Reviewed by Unknown on Sunday, September 23, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.