Top Ad unit 728 × 90

Movie zinalipa zaidi ya muziki - H-BABA

Mkali wa muziki wa Bongflava na tasnia ya filamu, Hamis Baba 'H- Baba', ametamka wazi kuwa katika kazi zote ambazo amekuwa akishiriki, sehemu ambayo angalau anaweza kuona fedha yake bila mizengwe ni katika filamu.
"Kusema ukweli japo hatupati malipo ya kivile, lakini katika filamu hakuna longo longo, uzuri wa filamu ni kwamba ukimaliza kazi yako ukikutana na msambazaji anakupatia fedha yako kulingana na mapato yako bila ya usumbufu," alisema.
"Lakini katika muziki unasubiri hadi uuze kopi na haujui zinazalishwa ngapi."
H. Baba anasema kuwa tangu aanze utayarishaji wa filamu, hajawahi kusumbuka kuhusu malipo baada ya mapatano.
Pamoja na yote hayo H-Baba ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Thamani Yetu’, amesema kuwa anatarajia kuachia albamu yake mpya Novemba mwaka huku ikiwa imepewa jina la ‘Shika Hapa Acha Hapa’, itakayokuwa na nyimbo 10.
Movie zinalipa zaidi ya muziki - H-BABA Reviewed by Unknown on Sunday, September 23, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.