Top Ad unit 728 × 90

Dimpoz abisha hodi na Video ya ‘Baadaye’.


Meneja wa msanii huyo Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema, Dimpoz ameifanyia ‘shooting’ video yake hiyo katika mandhari ya uhakika nchini Afrika Kusini, ambako kazi ya utayarishaji ilifanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Kwani Mshindi huyo aliyejinyakulia Tuzo mbili za Kili Music 2012, Ommy Dimpoz, anatarajiwa kufanya uzinduzi wa Video ya wimbo wake mpya wa ‘Baadaye’ ndani ya Ukumbi wa Club Maisha uliopo hapa Jijini.
Kwenye uzinduzi huo baadhi ya wasanii watamsindikiza Dimpoz, ni pamoja na Chegge Chigunda, Suma Mnazareth na Nas 3 na siku hiyo Dimpoz naye atakuwa kwenye muonekano tofauti na yule waliyemzoea.
Kwa sasa Msanii huyo, anatamba na mipini yake miwili, ni pamoja na ‘Nai Nai’ na ‘Baadaye’.
Dimpoz abisha hodi na Video ya ‘Baadaye’. Reviewed by Unknown on Friday, September 07, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.