Top Ad unit 728 × 90

Fid Q afikiria kuwapeleka kortini Orijino Komedi kwa kumchafua, lakini……….

Baada ya Orijino Komedi kumshutumu rapper Fareed Kubanda aka Fid Q kuwa amecopy na kupaste beat ya wimbo wake Danger, rapper huyo hajaridhika na hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kiasi cha kufikiria kutafuta mwanasheria ili awaburuze kortini waigizaji hao.

“Looking for a good lawyer dealing with defamation of character cases.. Contact us for details,” Fid alitweet jana. Baada ya kuona tweet hiyo, chanzo cha habari hii kilimpigia simu rapper huyo kutaka kujua kama kweli amedhamiria kulipeleka suala hilo kwenye sheria na yeye kusema kuna watu walimshauri afanye hivyo lakini ameamua kupuuzia.

Hata hivyo alisema suala hilo limemuumiza kwakuwa watu wasiofahamu masuala hayo wamemchukulia tofauti. “And you know one of the things that I hate nowdays is taking everything for granted. Unajua kilichoniuma ni kwamba ingekuwa Ulaya, watu Ulaya wanajua lakini sasa Bongo unapowaambia hivyo watu wanaamini hundred percent,” alisema.

Aliongeza kuwa amekuwa akipata ujumbe kupitia Facebook unaomkera kwakuwa watu wamepotoshwa na Orijino Komedi. Staa huyo wa ‘Sihitaji Marafiki, alikiambia chanzo cha habari kuwa atahitaji Orijino Komedi wamemuombe radhi rasmi kwa kuchafua jina lake.

Wiki hii studio iliyotengeneza beat hiyo iliamua kutoa tamko na kuwashutumu Orijino Komedi kwa kukurupuka kuongea kitu wasichokifahamu.

“Chofaco Records owns full copyright of the song Danger by Fid Q, produced by chobaray.Nyimbo ilirekodiwa November,2008,jiulizee nyimbo ilitoka mwaka gani?mziki wa USA sio sawa na mziki wa Bongo. Kuna tofauti kati ya mixtape songs and album songs also released tracks,non exclusive tracks and exclusive tracks,kabla orijino komedi kukurupuka na kuongea/kufanya vipindi vyao lazima mjue copyrights za kazi za watu,heshima na busara,kuuliza na kuelimishwa si ujinga.”
Fid Q afikiria kuwapeleka kortini Orijino Komedi kwa kumchafua, lakini………. Reviewed by Unknown on Thursday, September 13, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.