Top Ad unit 728 × 90

‘IRENE UWOYA’ NDANI YA FILAMU MOJA NA NYOTA WA MAREKANI ‘HALLE BERRY’ ???

WAKATI msanii Irene Uwoya akiendelea kufanya mchakato wa kutaka kushiriki kwenye filamu za kimataifa, tayari inadaiwa kuwa anatarajia kula shavu kubwa ambalo hajawahi kuliota la kushiriki filamu moja na msanii maarufu Halle Berry kutoka marekani.

Halle Berry ni moja ya wasanii mahiri kabisa ambao wana uwezo mkubwa kwani ameweza kuonesha uwezo wake kwenye filamu kama ‘Die Another Day’, Catwoman, New Year’s Eve, Monster’s Ball na nyingine nyingi.

Ishu ya Uwoya kushiriki ndani ya filamu moja na mwanadada huyo inadaiwa kuwa katika mazungumzo anayofanya nchini Uingereza mmoja ya wadau wakubwa ya tasnia hiyo kutoka Marekani ndiye aliyempa ishu hiyo baada ya kuona baadhi ya filamu alizocheza pamoja kujiamini kwake.

Uwoya alidai kuwa bado hajaamini kwani hajapewa ishu kamili na ameambiwa kuwa atajulishwa kwa njia ya email endapo kila kitu kitakuwa sawa kwa sababu ya ratiba ya Berry.

“Naweza kucheza filamu moja na Halle Berry, ingawa sijajua kama ishu hii inaweza kuwa kweli kwa sababu kama unavyojua kila kitu huwa kinaenda kwa ratiba siyo kama sisi bongo filamu tunajitolea bila hata kufuata ratiba,” alidai.

‘IRENE UWOYA’ NDANI YA FILAMU MOJA NA NYOTA WA MAREKANI ‘HALLE BERRY’ ??? Reviewed by Unknown on Tuesday, September 25, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.