Top Ad unit 728 × 90

“NILIKULA KIAPO KUWA SIWEZI KUMTAJA JINA STAA NILIYEMZUNGUMZIA KWENYE WIMBO WANGU WA ‘CHUKUA TIME’” – SUMA MNAZALETI…!!

WAKATI ngoma yake ya ‘Chukua Time’ ikiendelea kushika chati za juu, msanii Suma Mnazaleti, amesema kuwa watu wengi wamekuwa na hamu ya kutaka kumjua ni msanii wa bongo movie anayemzungumzia katika ngoma hiyo, lakini anashindwa kumtaja kwani tangu alipokuwa anaandika wimbo huo alikula kiapo kuwa hatokuja kumtaja jina kamwe.

Mnazaleti
alipotakiwa kuzungumza kuhusu jina la staa wa bongo movie ambaye anamzungumzia ndani ya ngoma hiyo, ndipo alipofunguka kuwa hawezi kumtaja mtu yeyote kwani ameshakula kiapo tangu alipokuwa anauandika wimbo huo.

Alidai kuwa watu wengi watu wana majibu yao lakini kwa upande wake hawezi kuzungumza chochote kwani anaamini hataki kumdhalilisha staa huyo kwa tabia zake za kumsubua kwenye simu wakati awali alikuwa anamuona kama kuku mchafu.


“Watu wengi wamekuwa na majibu yao kuwa ninayemuimba ni kati mtu fulani au fulani lakini kwa upande wangu ni nimekula kiapo cha kutomtaja niliyemzungumzia hivyo nawaomba mashabiki wangu wajue kwamba hata kwa mtutu siwezi kumtaja jina atabaki kuwa siri yangu”
alisema.
“NILIKULA KIAPO KUWA SIWEZI KUMTAJA JINA STAA NILIYEMZUNGUMZIA KWENYE WIMBO WANGU WA ‘CHUKUA TIME’” – SUMA MNAZALETI…!! Reviewed by Unknown on Monday, October 01, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.