Top Ad unit 728 × 90

‘WELLU SENGO’ MREMBO ANAYEKUJA JUU KATIKA TASNIA YA FILAMU BONGO…!!

MSANII wa filamu bongo Wellu Sengo, amesema kuwa baada ya kufanya vizuri kwenye kazi kadhaa sasa kung’arisha  filamu mpya ya ‘Vagabond’ ambayo amedai itakuwa moto wa kuotea mbali.

Filamu hiyo inatayarishwa na Producer
Mussa Mziba chini ya kampuni ya Zest Production, ambao ni mabingwa wa kutengeneza filamu Tanzania.

Sengo tayari ameshafanya kazi na kampuni kubwa zinazohusika na utengenezaji wa filamu kama Game 1st Quality pamoja na RJ company, huku akiwa ameshiriki kazi kama ‘Matilda’, ‘I know U’, ‘Twisted’ na nyingine kibao zote akiwa amecheza kama muhusika mkuu.

Wellu akiwa na Mzee chilo kwenye upigaji picha wa filamu ya Vagabond
Mwanadada huyo ambaye pia alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Vaa, Imba cheza kama Rihanna, alidai kuwa anaamini kwenye mzigo huo ameonyesha kiwango cha kimataifa kwa lengo la kufika mbali zaidi katika tasnia hiyo.
Filamu hiyo inatayarishwa na Producer Mussa Mziba chini ya kampuni ya Zest Production, ambao ni mabingwa wa kutengeneza filamu Tanzania.
‘WELLU SENGO’ MREMBO ANAYEKUJA JUU KATIKA TASNIA YA FILAMU BONGO…!! Reviewed by Unknown on Monday, October 01, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.