Top Ad unit 728 × 90

Tamasha la kitamaduni la Mwafrika mlangoni


Kwani  tamasha hilo limeandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali  ya Team Jambo, ambayo imeshapokea washiriki kutoka nchini Nigeria, Afrika Kusini, Kenya na Canada wakiomba kushiriki kwenye tamasha hilo kama watazamaji.
 
Si lingine bali ni lile Tamasha la Sanaa na Utamaduni wa Mwafrika, litakalohusisha vyakula vya asili na limeandaliwa kwa lengo la kukuza na kuenzi Utamaduni wa Mwafrika.
 
Nay Mwneyekiti wa Team Jambo, Augustin Namfua, alisema kwamna wameshakamilisha taratibu zote za kufanikisha tamasha hilo ambalo ni muhimu sana kwa wale wanaojishughulisha na shughuli za sanaa zikiwemo za Kitamaduni zaidi.
 
Mbali na hilo tamsha hilo litrakuwa ni la siku tisa, na kutakuwa na matukio sita muhimu ambayo yatahusika kulipamba, ikiwemo upatikanaji wa vyakula vya asili, shughuli za ngoma za asili na mdahalo wa wasanii ukiwahusisha wachongaji, wachoraji na wanamuziki.
 
“Lakini pia, katika siku za tamasha hilo kubwa kufanyika kwa wana sanaa na utamaduni hapa nchini, kutakuwa na siku moja ya matembezi, ambapo washiriki watakuwa wamevaa mavazi ya asili na kupita mitaa muhimu jijini Arusha,” alisema.
 
Alitoa wito kwa wasanii wa uchoraji, uchongaji na wajasiriamali wengine waliopo katika sekta hiyo ya sanaa, kujitokeza kujiandikisha kushiriki tamasha hilo ambalo ni muhimu kwao.
 
Tamasha hilo litawika ndani ya viwanja vya wazi vya mzunguko wa Kijenge na baadhi ya shughuli zitafanyika katika Hoteli ya Naura Spring na Via Via, katika siku maalumu ikiwemo ngoma za asili.
Tamasha la kitamaduni la Mwafrika mlangoni Reviewed by Unknown on Saturday, September 08, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.