Top Ad unit 728 × 90

‘AMINI’ KUMTAMBULISHA MPENZI WAKE SIKU YA FIESTA YA DAR OCTOBA 6…!!

BAADA ya kusumbuka sana na mapenzi yakiwemo ya kumpenda staa, msanii Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, amesema kuwa Octoba 6 mwaka huu siku ya tamasha la Fiesta, atamtambulisha mpenzi wake ambaye, anayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Linah.

Kwa hakika utambulisuho huo utakuwa wa aina yake kwani mashabiki wake wengi wanajua jamaa bado anamzimia
Ndege Mnana huku wakiwa hawaelewi kitu kilichowafanya hadi wakaachana ingawa bado wana mahusiano mazuri kwenye kazi.

Amini aliumpa mtandao huu mchongo huo ili kuwataliafu mashabiki wake kuwa alikuwa kimya kwenye suala zima la mapenzi baada ya kuumizwa sana, lakini sasa anaamini ni wakati muafaka wa kumtambulisha kimwana wake.


Alisema kuwa mpenzi atakayemtambulisha siku hiyo ndiye mke mtarajiwa kwani haoni sababu ya kuendelea kuumizwa na mapenzi wakati muda wa kuvuta jiko umekaribia.


“Sihitaji kumtambilisha kama mpenzi bali ni kama mke kwa sababu naamini anavyonipenda ni kiasi cha kujivunia kwa sababu mara zote huwa nazungumza naye mambo ya ndoa na yupo radhi kuishi na mimi kwa shida na raha,”
alisema Amini.

‘AMINI’ KUMTAMBULISHA MPENZI WAKE SIKU YA FIESTA YA DAR OCTOBA 6…!! Reviewed by Unknown on Tuesday, October 02, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.