Top Ad unit 728 × 90

‘Ben Pol’ aja na ladha tofauti

Lengo la kubadili mazingira ya kufanyia kazi yake ya video ya wimbo wake, ni kuwavutia mashabiki katika kazi zake.
Ni yule Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini, Bernard Paul ‘Ben Pol’ anajiandaa kwenda jijini Tanga kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Pete’, ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio hivi sasa.
Alisema ili awavutie mashabiki wake ameamua kufanya vitu tofauti, kwani wasanii wengine wanapenda kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya video.
Alisema kwa hapa nchini kwetu, kuna mikoa mingi ambayo ina mvuto na hii itakuwa njia pekee ya kuwavuta mashabiki katika kazi zake.
Mbali na hilo video hiyo anaifanyia chini ya Kampuni ya Ogopa Records ya nchini Kenya, ambapo tayari wameanza kuandaa mazingira kwa ajili ya kazi hiyo.
Kwa sasa mwabanmuziki huyo anatamba na vibao vyake kama ‘Maneno’, ‘Nikikupata’, ‘Number One Fun’ na vingine ambavyo vinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

‘Ben Pol’ aja na ladha tofauti Reviewed by Unknown on Tuesday, October 02, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.