Top Ad unit 728 × 90

“NIKIENDA KUSALIMIA WAZAZI HUWA NAVAA MAVAZI YA KILOKOLE ZAIDI” – LINAH…!!

KIMWANA ambaye hivi sasa yupo kwenye mahusiano na jamaa ambaye anayeishi nchini Marekani, Linah Sanga, amedai kuwa huwa anapoenda nyumbani kwa wazazi wake huwa navaa nguo ndefu tena za kilokole zaidi ili asije kuwaudhi wazazi wake ambao wamemkuza katika maisha hayo.

Msanii huyo anapenda kuishi kizungu baada ya kuigia kwenye muziki, ingawa anadai kuwa hawezi kusahau maisha ya kidini aliyokuwa anaishi awali ambayo yalikuwa yanamfanya avae nguo za heshima tofauti na sasa.


Linah
alidai kuwa tangu alipoachana na wazazi wake maisha yake yamekuwa tofauti kwani muziki kwa upande fulani umebandilisha maisha yake, kuanzia kwenye mavazi tabia na hata lifestyle.

“Napozungumza tabia haimanishi nimekuwa muhuni hapana, bali awali nilikuwa sijuani na watu maarufu lakini sasa nimekuwa nao karibu na kuna baadhi ya vitabia nimekuwa navyo lakini si kwa ubaya,”
alidai.

Msanii huyo aliongeza kuwa wazazi wake wamekuwa wakimsihi sana kuvaa nguo zile zile za zamani lakini haoni kama zina nafasi kwa sasa kutokana na career aliyoichagua.

“NIKIENDA KUSALIMIA WAZAZI HUWA NAVAA MAVAZI YA KILOKOLE ZAIDI” – LINAH…!! Reviewed by Unknown on Monday, October 08, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.