Top Ad unit 728 × 90

‘SNURA’ KUVISHWA PETE YA UCHUMBA HIVI KARIBUNI, ADAI IKITOKA HIYO HATUA INAKUJA YA NDOA…!!

MASTAA wengine wakiwa wanavishwa pete za uchumba na kuvuliwa, msanii Snura, amebwabwaja kuwa hivi karibuni anatarajia kuvishwa pete na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye naye ni mwanamuziki, ingawa hakutaka jina mwaume huyo liwekwe hadharani kwani siku hiyo itakuwa ya kushtukiza.

Hata hivyo alipoulizwa kuwa vipi hayawezi kutokea kama ya wale wengine ambao walivishwa kwa mbwembwe na mwisho wa siku mambo yakawa mabaya na aibu juu, alijibu kuwa hao ni wao na yeye ni mwingine hivyo haoni kama yanaweza kutokea mambo kama hayo ya ajabu.


Alidai kuwa hata baadhi ya rafiki zake hawamjua mwanaume huyo ambaye atafunga naye ndoa, kila kitu kutakuwa na kushangaza kwani hata wale wengine ambao walikuwa wanampiga vijembe watabaki midomo wazi.


“Mambo ndiyo kwanza yanaanza hivyo siku za usoni navishwa pete na haitakuwa ya mbwembwe kama wale wengine, lakini kikubwa nachowaomba mashabiki wangu ni kwamba nimeshindwa kumtaja mpenzi wangu kwani na yeye ni staa mkubwa bongo kwa sababu anaimba na kitu hiki kitakuwa cha kushtukiza sana,”
alisema.

‘SNURA’ KUVISHWA PETE YA UCHUMBA HIVI KARIBUNI, ADAI IKITOKA HIYO HATUA INAKUJA YA NDOA…!! Reviewed by Unknown on Monday, October 08, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.