Top Ad unit 728 × 90

Nimeamua kufanya SIASA - Nature

Toka pande za TMK, msanii ambaye haishi kupendwa hata akikaa kimya miaka kadhaa bila kutoa ngoma, namzungumzia Juma Kassim Nature ameweka wazi kuwa sasa ameamua kujishughulisha na siasa

HAYA NDIO MANENO YAKE
"Ingawa bado nipo kwenye muziki ila mimi ni mwanachama wa chama kimoja ambacho siwezi kukitaja kwasasa, na nina mpango wa kugombea jambo fulani hivi punde' anaanza kwa kusema.
"Licha ya kwamba mimi mwenyewe napenda kujihusisha na siasa, lakini bado wapenzi wangu wengi wananitaka nigombee jimbo la Temeke huko Mbagala ninakoishi ili niweze kuwaongoza, nakubaliana na hilo na ndio maana nimeliweka katika ratiba za maisha yangu" anasema.
Nature anaweka bayana kuwa hana woga wowote na vikwazo mbalimbali ambavyo hutokea katika uongozi na anaamini kuwa ana karama hiyo na pia anapendwa na wengi.
Je bwana huyu unahisi atakuwa shabiki wa chama ganiiiii??

Nimeamua kufanya SIASA - Nature Reviewed by Unknown on Friday, October 05, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.