Top Ad unit 728 × 90

POLISI WAWANASA WAUAJI WA KAMANDA BARLOW MWANZA

Manumba akitaja majina ya wahusika pembeni kushoto ni IGP Mwema
Majina ya watu matano  wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow yametajwa rasmi leo jijini Mwanza.

Akitaja majina hayo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba,  amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo hatimaye wahusika kukamatwa...

Majina ya wahusika hao kuwa ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye inatajwa kuwa ndiye aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48),  Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa katika jiji la Dar es Saalm.

 Alisema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi linasaka wengine. Lakini hakuna sababu iliyotokana na mauaji hayo ambayo imeelezwa mpaka sasa na jeshi hilo

Liberatus Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Minazi mitatu huko Kitangiri wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji. moja 
Baadhi ya Wananchi, Waandishi na Polisi wakifuatilia kinachojiri ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza jioni ya leo.
 

 
POLISI WAWANASA WAUAJI WA KAMANDA BARLOW MWANZA Reviewed by Unknown on Friday, October 26, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.