Top Ad unit 728 × 90

‘SHILOLE’ AKANA KUWA NA MAHUSIANO YA MAPENZI KIMYA KIMYA NA ‘OMMY DIMPOZ’…!!



INASEMEKANA kuwa kimwana anayetesa kwenye filamu na muziki Shilole na Ommy Dimpoz, wapo katika mahusiano ya chini chini na hawataki kuyaweka wazi kwa kuogopa midomo ya watu.

Chanzo kilicho karibu na msanii Shilole kilitoa fununu ya ishu hiyo kwa kudai kuwa wasanii hao mara nyingi wamekuwa wakikutana nyakati za usiku na awali kabisa walikuwa kama marafiki lakini kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ukaribu wao uliongezeka na kuanzisha mahusiano.

Mdaku huyo alidai kuwa hakuna mtu anayejua wasanii hao kama wana mahusiano, kwani wanafanya siri kwa kuogopa vyombo vya habari na hata wanapotaka kuonana huwa wanatumia usafiri wa kukodi kwa sababu tayari magari yao yanajulikana.

“Ishu ambayo mimi naijua ndiyo hiyo kwa sababu ukaribu wao umekuwa mkubwa na sijui kama wanaweza kusema si wapenzi, kuna sehemu tata ambazo nimewahi kuwakuta na wakaniambia nisitoe ishu hiyo kwa mtu yeyote,” kilidai chanzo hicho.

Hata hivyo chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kudai kuwa zipo tabia ambazo mara nyingi Shilole amekuwa akizifanya, kama za kutoka usiku lakini sasa hana ishu hizo na inadaiwa kuwa Dimpoz ndiyo aliyemshauri na kumsihi atuliye na kama wanataka kutoka basi lazima wawe wote.



Aliongeza kuwa yeye anatoka na msanii mwingine kabisa ambaye mara zote watu wamekuwa wakimuona nae.

“Sina mahusiano ya kimapenzi na Dimpoz na huyo mtu anayetaka kuzungumzia ishu ambayo haipo anamatatizo yake, Dimpoz ni rafiki yangu sana tena kwa sababu ni msanii mwenzangu na hakuna kikubwa ambacho kinaendelea kati yetu,” alisema Shilole.


‘SHILOLE’ AKANA KUWA NA MAHUSIANO YA MAPENZI KIMYA KIMYA NA ‘OMMY DIMPOZ’…!! Reviewed by Unknown on Saturday, October 13, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.