Top Ad unit 728 × 90

‘MR CHUZI’ KUACHIA FILAMU MPYA ‘MKALI MO’, KUPATIKANA SOKONI KUANZIA JUMATATU IJAYO…!!

Kampuni ya Tuesday Entertainment, inatarajia kuanza kusambaza filamu yake ya ‘Mkali Mo’, ambayo itakuwa sokoni kuanzia Jumatatu hii ya Octoba 15 mwaka huu.

Hata hivyo kampuni hiyo pia baada ya kwenda sokoni kazi hiyo, wiki hiyo hiyo unakuja ujio mpya wa season ya pili wa tamthilia ya ‘Jumba la Dhahabu’, hivyo kwa wale wote waliokuwa wanaifuatilia kazi hiyo ni wakati wao wa kuanza kuitazama na kujua nini kilichoendelea pale ilipoishia.

Ujio wa filamu hii unaweza kuwa tofauti kidogo kwani watu wamezoea kumuona King Majuto akicheza komedi lakini safari hii amecheza kama baba wa msanii Niva, na hajaonesha ukomedi wowote kama watu walivyozeoa kumuona kwenye kazi mbalimbali.

Niva naye amacheza kama mtoto wa uswahilini aliyejaa vituko kitu ambacho kinazidi kuipa chati kazi hiyo kwani wasanii wote waliocheza humu wameonesha utofauti mkubwa kutokana na nafasi zao wanazocheza siku zote.

“Lengo letu ni kuonesha utofauti wa kazi na mashabiki wajue tunafanya nini, lakini kubwa tunahutaji kuelimisha na kuburudasha na hilo ndilo kubwa zaidi kwani hatuhitaji mtu apotee hivyo akitazama kazi hii atajifunza mambo mengi,” alisema Mr Chuzi.
Download Mkali Moo The Sound Track iliyoimbwa na Niva

‘MR CHUZI’ KUACHIA FILAMU MPYA ‘MKALI MO’, KUPATIKANA SOKONI KUANZIA JUMATATU IJAYO…!! Reviewed by Unknown on Saturday, October 13, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.