Top Ad unit 728 × 90

Mchumba wa The Game ajisifu kuyatibu maumivu aliyoyapata (Game) kwa 50 Cent.

Inawezekana kweli kabisa kuwa mapenzi yanapoanzia ndipo ugumu unapoishia, na aliyesema Love is a cure huenda kwa hii story akawa right.

Mchumba wa the West Coast rapper Game, Tiffney Cambridge hivi karibuni ameelezea uhusiano wake na mkali huyo wa michano na kwamba walikutana muda mfupi baada ya Game kutoka G-Unit katikati ya miaka ya 2000.

Mrembo huyo ameelezea mahusiano yao yalivyoanza na kushamiri na kwamba walikutana wakiwa katika wakati mgumu sana na walisaidiana kusolve matatizo yao kwa kutumia mapenzi tu. Walivyokutana sasaa..., ni story nzuri hasa ukimjengea picha Game aliyolainika kwenye mikono ya mrembo huyu.

“kupitia mtoto wa dada angu, dada yake Game alikua anatengeneza nywele kwenye barbershop yake, kwa hiyo nilikuwa naenda kutengeneza nywele pale, kwa hiyo nilikuwa namuona Jayceon pale,” alisema Cambridge alimtaja Game kwa jina lake la kuzaliwa.

Mrembo huyo alielezea kuwa Game alikuwa kama anamuwindawinda kwa kwa maneno flani ya uchokozi hata walipokuwa wanakutana nje ya maeneo ya barbershop hiyo, “can I take you out? and all that kind of stuff”.

Cambridge aliendelea kufunguka, “...tulikuwa na shangwe kibao tukiwa pamoja. Wakati mama yangu alipofariki alinisaidia sana kunituliza, na mimi nilimsaidia alipokuwa anatoka kwa mara ya kwanza G-Unit. Kiukweli tulidevelop urafiki wa kipekee japokuwa ilikuwa ndio kama kufall in love hivyo.” Wakati Game anatoka G-Unit alikuwa na challenge sana na media zilimuandama na mengi ya kumuumiza yalitoka kwa 50 Cent aliyemuona kama a rebel.

Game na Cambridge sasa ni wachumba na kwa mujibu wake Game Alishapropose kwake mara nyingi na wakati mwingine akiwa amekasirika kabisa lakini Game alipenyeza maneno mazuri ya kimapenzi akitaka awe mkewe wa halali, na hii ilisababisha wakati mwingine amkatalie kwa sababu alikuwa amekasirika.

hivi karibuni Game alielezea kuwa amejaribu sana kumuweka mbali mchumba wake huyo na media kwa sababu hataki kumuumiza, "nilimuweka mbali kwa sababu nilifeel ingeweza kumuumiza au kumdhuru" alisema Game. "Na sikuwa tayari naye hakuwa tayari, ni mengi ya kudeal nayo na kwa upande mwingine, I was trying to keep it player.”

Mchumba wa The Game ajisifu kuyatibu maumivu aliyoyapata (Game) kwa 50 Cent. Reviewed by Unknown on Wednesday, November 21, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.