Top Ad unit 728 × 90

Snare wa East Coast awa producer wa filamu, tazama trailer ya movie aliyofanya – Shujaa

Kwa muda mrefu aliyekuwa member wa kundi la East Coast Team, ECT, rapper Snare, amekuwa kimya na shughuli za muziki lakini ameamua kuelekeza nguvu zake kwenye filamu.Kwa sasa Snare ni mtayarishaji wa filamu chini ya kampuni iitwayo Afronode Film na December 1, 2012 anatarajia kuzindua filamu iitwayo SHUJAA…

check out trailer yake hapa


Amani ni mmoja wa vijana aliyeguswa na kitendo cha Raisi JAKAYA MRISHO KIKWETE cha kuamua kupima VVU hadharani.Naye kuanzia hapo alijiwekea utaratibu wa kufanya hivyo kila baada ya miezi mitatu, na kwa bahati nzuri alikuja kufanya kazi katika shirika linaloshugulika na na kupima VVU na Ushauri nasaha. 

Siku moja alikutana na binti mzuri Fransisca akiwa katika mazingira ya kujiuza (changudoa). Alimuona ni mzuri sana akampenda, na akataka kujua zaidi .Hadithi ya maisha ya yule msichana ndio yanamfanya amani awe na imani zaidi .Lakini jambo moja linatatiza kati yao je yule msichana ni salama? hakuna kinachoweza kufumbua fumbo hili zaidi ya kwenda kupima kitu ambacho Francisca hakuwa tayari kutokana na idadi ya wanaume aliotembea nao. 

Ugumu wa jambo hilo haumkatishi tamaa amani, hatimaye anafanikiwa kuokoa maisha ya msichana huyo. Na kutimiza ndoto zake za kuwa shujaa kama Raisi Jakaya Kikwete.
Snare wa East Coast awa producer wa filamu, tazama trailer ya movie aliyofanya – Shujaa Reviewed by Unknown on Monday, November 26, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.