Top Ad unit 728 × 90

The Game amtishia 50 Cent, amuita Zombie, adai ataiua G-Unit kwa nguvu mara mbili zaidi ya ile ya kwanza, ni baada ya ‘My Life Diss’...angalia video ya Game akitiririka.

The West Coast rapper Game ambae alikuwa ni member wa zamani wa G-Unit hakukawia kujibu Diss iliyotupiwa yeye na Young Buck kwenye ngoma mpya ya boss wao wa zamani 50 Cent ‘My Life’.

Game amesema anajiona kama anaanza kufatilia kwa karibu ile hard hitting yake “300 Bars” aliyotoa mwaka 2005 kwa ajili ya kudiss G-Unit.

Game ambae nae aliwahi kutoa ngoma inayoitwa ‘My Life’ akiwa na Lil Wayne alipiga interview na Power 106 huko States na akaanza kwa kusema yeye pia aliwahi kuwa na wimbo unaoitwa ‘My Life’, then bila kutafuna maneno akafunguka zaidi.


“Labda ana kitu ambacho anataka kutuambia, unajua, kuhusu maisha yake ya siri,” alifunguka Game baada ya kukiri kuusikia huo wimbo wa 50 Cent. “Hakuna mtu anaemuogopa 50. Tuwaulize watu. That’s really the best he can do. You know what I’m saying? Buck yuko jela, hali yake ni hiyo, hawezi kujitetea kutoka huko...Every now and again, unapata hii movie ya Zombie ambapo haijalishi ni mara ngapi unawashot, wanaendelea kuamka...Freestyle yangu ya mwisho ilikuwa kama ‘500 Bars’ na ilikuwa na kama na dakika 26. Freestyle iliyoiua G-Unit, kila kitu, record lebel, nguo ni ‘300 Bars’ na natakiwa kwenda na kuifanya mara mbili ya hapo niseme kiukweli kile nachotakiwa kusema. Kuna mengi ya kusema.” That’s Game.


Kwenye ‘My Life’ ambayo ni ngoma mpya ya 50 Cent akiwashirikisha Eminem na Adam Levine, mistari ya kwanza ambayo inawadiss Game na Young Buck direct kwa kuwataja majina ni hii hapa.


"Yeah, 03, I went from back filthy to filthy rich /Man, the emotions change so I can never trust a b*tch/I tried to help n*ggas get on, they turned around and spit/Right in my face, so Game and/Buck, both can suck a d*ck/Now when you hear 'em it may sound like it's some other sh*t/Cause I'm not writing anymore, they not making hits".


Baada ya Game kutoka G-Unit mwaka 2003 hivi alianzisha harakati nyingi za kuimaliza G-Unit na kutoa freestyle nyingi kama diss kwa G-Unit lakini akazipa jina la ‘G-UNOT’ harakati zake ambazo watu wa mtaa walitoa hadi t-shirt zenye maandishi hayo... ‘G-UNOT’.


Hii ndio interview ya Game kuhusu diss ya 50 Cent
The Game amtishia 50 Cent, amuita Zombie, adai ataiua G-Unit kwa nguvu mara mbili zaidi ya ile ya kwanza, ni baada ya ‘My Life Diss’...angalia video ya Game akitiririka. Reviewed by Unknown on Thursday, November 29, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.