Top Ad unit 728 × 90

Toni Braxton Afilisika!!!

Mwanamuziki mkali wa R&B aliewahi kutamba na ngoma zake kama Unbreak My Heart Na Nyingine amefunguka hivi karibuni ametangaza kufilisika. Toni ameseam, vitu vilivyomfanya kufilisika ni pamoja na manunuzi mabaya ya vitu vya nyumbani na jikoni ambavyo vimekuwa havina umuhimu mkubwa.

Kufilisika kwake kulianza kuonekana kwa mara ya kwanza mwaka 1998 na kuwashangaza sana mashabiki wake hasa kwa star mkubwa kama huyu ambae album yake iliuza kwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 170. Toni Braxton, mwenye miaka 45, pia amesema, label yake ya LaFace Records ilichukua hela nyingi bila yeye kuona mapato yoyote.

Toni pia, aliendelea kufunguka kwa kusema, pesa nyingi zilitumika kwa kununua vitu vya nyumbani ambavyo anavipenda sana na kwamba yeye yuko tofauti. Akiongeza mwishoni, Toni alisema amejifunza mengi zaidi kuhusu kutunza pesa kuanzia sasa na atafanya lolote ili kuweza kujipanga kimatumizi ili aweze kurudi sawa kifedha.

Toni Braxton Afilisika!!! Reviewed by Unknown on Wednesday, December 05, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.