Top Ad unit 728 × 90

VIDEO: Chek out Show ya Ommy Dimpoz yavurugika Dodoma kutokana na skendo ya kumtukana Marehemu Ngwea

Ile skendo ya Msanii Ommy Dimpoz kumtolea maneno ya kejeli na matusi aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea imemtokea puani mbana pua huyo mara baada ya kutinnga Dodoma katika ile Tour ya washindi wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards na kushindwa kufanya kile alichokusudia kukifanya.

Ommy Dimpoz kama kawaida yake unaweza kuamini hata hayo maneno ambayo anayakanusha ya kumtukana Ngwea yasikuingie akilini pale ambapo alisimama na kutoa maneno machache tu tena hata bila ya kuwa na msisitizo wowote ama kuonesha kweli alisingiziwa. Msanii huyo aliweza kutamka tu kifupi kwa kuwaambai mashabiki kuwa "Mimi nakiri kwamba sikumtukana Albert Mangwea" baada ya kutoa maneno hayo alimruhusu Dj aweze kuendelea na yake na show ikaanza.

Lakini mara tu baada ya wimbo wake wa kwanza kuisha uliofuata wa pili alijikuta akiwa na kazi mbili yaani kuimba na kukwepa chupa zilizokuwa zikirushwa na mashabiki ambao wote walikuwa wakimtaka aondoke haraka jukwaani na kama sio nguvu ya ziada ya walinzi kumlinda kwa kuzuia chupa hizo na kumshawishi ashuke haraka huenda hata angepata majeraha asoyatarajia, ilibidi akubali matokeo kwamba mashabiki hawamtaki na ndipo aliposhuka hukua akiwaacha madancer wake wakiendelea kuumalizia wimbo wake kwa kucheza kwa aibu kabla nao hawajamfuata boss wao.

Tour hiyo ya Kili Music ilizinguliwa Jioni ya Jumamosi tarehe 22/06/2013 mkoani Dodoma na itafuatiwa na mkoa wa Tanga na kuendelea na mikoa mingine.

Angalia video jinsi mashabiki walivyokuwa wakimtaka ashuke haraka jukwaani....
VIDEO: Chek out Show ya Ommy Dimpoz yavurugika Dodoma kutokana na skendo ya kumtukana Marehemu Ngwea Reviewed by Unknown on Sunday, June 23, 2013 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.