Top Ad unit 728 × 90

Bob Haisa atimiza mwaka mmoja tangu aanze kutoa ngoma mpya kwa kila mwezi [Habari]


"Leo ni siku muhimu kwangu kwani mwaka mmoja unatimia tangu nianzishe rasmi utaratibu wa kuachia ngoma zangu kupitia mitandao, nakumbuka wimbo wa amechoka wakukaya video ndo ulifungua dimba kwa kuingia mtandaoni kwa 'TASHTITI" nyingi, licha ya kwamba wimbo huu uliwekwa mapema na director Louis Bwenge. Tarehe ya leo ndo ulisambazwa rasmi na kuwafikia mafans wangu wengi hali iliyoamsha ari zaidi na kunifanya nitangaze rasmi kwamba kila mwezi nitaachia wimbo mmoja zoezi ambalo limefana vyema ndani ya mwaka mzima. Zaidi ya nyimbo kumi na mbili zimekwenda hewani na zimepokelewa poa sana na ma Djs na wanahabari pamoja na mashabiki na wapenzi wa muziki wangu,hii imekua njia nzuri na rahisi kwangu kuwafikia watangazaji wa Radio na Tv mbalimbali kwakua wanazipata ngoma kwa muda muafaka na kuzitendea haki.
Changamoto kadhaa nimekutana nazo lakini hazikuathiri zoezi hili kwani malengo hayajakwama na ndo kwanza safari inaanza, niwe muwazi kwa kuwashukuru wote walioniunga mkono katika zoezi hili endelevu linalohitaji ushirikiano na uungwaji mkono pia napenda kuwahakikishia wadau wangu kwamba kila tarehe 15 ya kila mwezi nitaendelea na zoezi la ngoma mpya moja baada ya moja. Ahsanteni Sana" Bob Haisa Yes.
Bob Haisa atimiza mwaka mmoja tangu aanze kutoa ngoma mpya kwa kila mwezi [Habari] Reviewed by Unknown on Wednesday, June 25, 2014 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.