PHD SASA 'AMTAKA' JACK WA CHUZI
BAADA ya msanii wa filamu Jackline Pantezel ‘Jack wa Chuzi’,
kuwatetea wanawake juu ya kuchukuliwa kama samaki na msanii Hemed
Suleiman ‘P.H.D’ sasa staa huyo naye ameamua kufunguka na kudai kuwa
hakupanga kutembea na mwanadada huyo lakini sasa ajiendae kutoka naye
kwani amejipendekeza kwa kuzungumzia kauli yake.
Awali kabisa Hemed alidai kuwa endapo akiamua kuoa basi atafanya
mchakato kama wa BSS wa kufanya mchujo na kupata yule mwanamke bora
zaidi na mrembo kitu ambacho kilimfanya ‘Jack wa Chuzi’ kuinuka na
kumtaka Hemed awaombe radhi wanawake kwani asiwachukulie kama samaki
wanaopatika kilahisi tena kwa wingi.
Kauli hiyo ya Jack inaonekana kumtokea puani kwani mambo yanazidi
kuwa magumu ambapo PHD anadai kuwa atafanya juu chini ili tu amuonesha
Jack kuwa yale anayoyazunumza anauwezo wa kufanya na hata yenye anaweza
kuwa mmoja kati ya wanawake watakaohitaji kuolewa naye ingawa hana
vingezo anavyovihitaji.
“Sikupenda kauli ya Jack kwani namchukulia kama msanii mwenzangu
ambaye nafanya naye kazi lakini kitendo chake cha kupinga kauli yangu
kumenifanya niwe na hamu ya kutoka naye ili tu ajue kwamba nina uwezo wa
kutoka na mwanamke yeyote tena pale ninapomuhitaji tu,” alidai Hemedi.
Hata hivyo mwandishi wa ishu hii baada ya kumtafuta muhusika wa pili
wa kideo hiki Jack, alidai kuwa Hemedi hawezi kufanya kitu chochote
kwake na anamchukulia kama mtoto anayekuwa na kuanza kujua wanawake
hivyo haoni kama anaweza kuleta madhara.
“Hemed ni mtoto hivyo namchukulia kama ndo kwanza anawajua wanawake
sasa, kwa sababu mtu mzima awezi kuanza kujisifu kuwa anaweza kurembea
na kila mwanamke, kwani tayari ameshapitia huko asa kwa huyo ndo kwanza
anawajua wanawamke siyo makosa yake anahaki ya kusema hivyo,” alisema
Pentzel.
PHD SASA 'AMTAKA' JACK WA CHUZI
Reviewed by Unknown
on
Monday, September 10, 2012
Rating:
No comments: