Prezzo: Nitautumia ubalozi wa One Campaign kusaidia wenye njaa na si kimaslahi
Mshindi wa pili wa Big Brother Africa Stargame, Jackson
Makini aka Prezzo amesema kazi yake kama balozi wa One Campaign ni kukuza
uelewa kuhusu balaa la njaa na matatizo yanayowakumba waafrika maskini na sio
kwaajili ya kujinufaisha kiuchumi.
“Sisi tuko poa you know, tukitoka hapa tunaenda kupata zege
but kuna sehemu yaani Afrika ambapo hawapati msosi kabisa,” Prezzo alisema
kwenye kipindi cha Mkasi cha EATV kilichorushwa jana usiku
Alisema anategemea kuanza majukumu yake kama balozi wa
kampeni hiyo katikati ya mwezi huu ambapo ataripoti kwenye makao makuu ya One
Campaign mjini Washington DC.
“Washington DC nitakaa kama wiki na nusu, orientation you
know, wanipe bendera yangu ya gari,
wanipe passport yangu.”
Alieleza kuwa akiwa Washington atatengeneza t-shirt zake
alizozipa jina la ‘Swagga Farmer’ na ndipo atakapoelekea jijini New York kwenye
show ya Jay-Z.
Prezzo aliongeza kwa kudai kuwa kama balozi wa One Campaign
anataka kuona analeta mabadiliko fulani katika bara la Afrika na kama kampeni
hiyo ikifanikiwa kupunguza njaa katika maeneo duni barani humu, atajipongeza.
Prezzo: Nitautumia ubalozi wa One Campaign kusaidia wenye njaa na si kimaslahi
Reviewed by Unknown
on
Tuesday, September 11, 2012
Rating:
No comments: