Ubalozi wa Marekani walipa shavu Hip-Hop Darasa la Fid Q
September 8 mwaka huu, kaimu afisa wa masuala ya kijamii
Roberto Quiroz II na afisa msaidizi wa masuala ya kitamaduni Shamsa Suleiman wa
ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, waliungana na rapper Fareed Kubanda aka
Fid Q kwenye Hip Hop Darasa jijini Dar es Salaam lililohudhuriwa na washiriki
vijana zaidi ya 100.
Katika ziara hiyo, ubalozi wa Marekani ulilisaidia darasa
hilo zaidi ya vitabu 100 na mipira ya kikapu kwa niaba ya watu wa Marekani.
Tunafundishwa na Fid Q maana halisi ya mafanikio, kurudisha
kwa jamii kwa kuelewa kuwa kila mtu ana thamani kubwa na umuhimu, kuhakikisha
kuwa vijana wa leo wanapokea mafunzo na elimu muhimu kwa maisha yao ya
baadaye,” alisema Quiroz II.
“We are honored to partner with Fid Q and his team in this
noble and urgent endeavor. books and basketballs on behalf of the American
people to participants.”
Fid Q alianzisha mradi huo kuwafundisha watoto, vijana na
wale wanaopenda kuwa wasanii kupromote vipaji vyao, kuwapa elimu na kuwaelekeza
mienendo sahihi katika jamii wanayoishi.
Darasa hilo huwafundisha vijana kuzungumza masuala
mbalimbali kupitia muziki na sanaa na kutoa mitazamo na michango yao kwenye
jumuiya zao kwa ushirikiano na kufanya kazi kama timu na wengine.
Ubalozi wa Marekani walipa shavu Hip-Hop Darasa la Fid Q
Reviewed by Unknown
on
Tuesday, September 11, 2012
Rating:
No comments: