Cassidy asema Meek Mill bado hastahili ‘a diss record’.
Kwa wiki chache zilizopita rapper kutoka MMG Meek Mill na rapper wa muda mrefu kidogo kwenye game Cassidy, wamekuwa wakipigana madongo ya chini kwa chini na wajuzi wa mambo wanasema tayari hiyo ni ishara ya nia ya wazi ya Meek Mill kuhitaji battle na Cassidy.
Akipiga exclusive Interview na mtandao wa AllHipHop, Cassidy amepata nafasi ya kuzungumzia asili ya ishu hiyo na kote ilikoanzia.
Alipoulizwa kama track yake mpya “Diary of a Hustla” ni diss kwa rapper huyo mwenye asili ya Philadelphia, Cassidy amesema Meek Mill bado hajafanya chochote kwenye game hii kinachostahili ‘a diss record’ na kuonya kwamba kama Meek Mill mwenyewe anaona hiyo ngoma ni diss kwake basi anatakiwa kujibu kwa level za “Nas”.
“Kama nimefanya ‘a diss record’ kwa ajili ya Meek Mill basi inatakiwa iwe katika level nyingine na sio chini ya hapo…inatakiwa iwe direct na isiwe kazi ngumu kutambua ni nani hasa namdiss…lakini sioni kama ana chochote cha maana ambacho amekifanya katika huu muziki kinachonifanya nitengeneze diss track kwa ajili yake…anatakiwa afanye ngoma na anizungumze kipuuzi sana ili apate a diss record kutoka kwangu…na namshauri asifanye nisemavyo mimi kwa sababu kama akiingia ulingoni na mimi itakuwa tatizo kweli…anajua uwezo wangu…na anajua pia ninavyoweza kuingia”…amesema Cassidy.
Cassidy asema Meek Mill bado hastahili ‘a diss record’.
Reviewed by Unknown
on
Friday, November 23, 2012
Rating:
No comments: