Wiz Khalifa atoa credits kwa rapper asiyefahamika sana nchini marekani ‘Devin The Dude’.
Katika interview yake na OTHER personality Nardwuar, rapper toka Pittsburgh Wiz Khalifa, amechukua muda kidogo kutoa shot out kwa emcee asiyefahamika sana Devin The Dude, msanii ambaye Wiz amesema anachukua mguso wa kipekee kwake.
Topic kuhusu Devin The Dude na muziki wake ilikuja baada ya Wiz Khalifa kuzungumzia mkono mkali wa rapper huyo uliotengenezwa na Dj Premier “Doobie Ashtray”
Rapper huyo anayewakilisha Taylor Gang pia amemzungumzia Devin The Dude kama mmoja kati wa wasanii ambao wanachukuliwa poa sana.
“Yo…huu ni wimbo mkali sana wa kuvutia bangi…Devin The Dude ni mtu wa muziki japo….jamaa anachukuliwa poa sana…lakini asikwambie mtu muziki wake na namna anavyopita ndo hasa kinachonikosha…shout out to Devin…sijawahi kusema hili wazi..lakini kiukweli mchizi anajua”…alisema Wiz.
Wiz Khalifa kwa sasa anajiandaa kudondosha mzigo wake mpya ambao umekuwa ukisogezwa mbele kila inapokaribia muda uliotangazwa kutoka. Mara ya mwisho Wiz mwenyewe alitangaza kuachia mzigo huo “O.N.I.F.C.” Dec 4 mwaka huu.
Wiz Khalifa atoa credits kwa rapper asiyefahamika sana nchini marekani ‘Devin The Dude’.
Reviewed by Unknown
on
Friday, November 23, 2012
Rating:
No comments: