MB Dogg kurudi na AMENIMISS!
Baada ya kimya kirefu nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mb Doggy anajipanga kuachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Amenimiss’.
Akizungumzia hilo na Darhotwire jana kwa njia ya simu, Dogg alisema
yupo katika hatua za mwisho za uaandaaji wa ngoma hiyo ambayo itakuwa na
ujumbe mzito kwa jamii pamoja na wapenzi wa kazi zake.
“Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu nimeamua kuja na ngoma hiyo
ambayo naamini itakuwa moto wa kuotea mbali kwa mashabiki wangu kutokana
na ubora wa kazi yenyewe,” amesema Mb Doggy.
Dogg amewaomba mashabiki wake wakae kukaa tayari kuipokea ngoma hiyo.
Mb Doggy alishawahi kutamba na ngoma zake kama, Si Uliniambia,
Inamaana na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri kwenye
tasnia ya muziki wa bongo fleva.
MB Dogg kurudi na AMENIMISS!
Reviewed by Unknown
on
Thursday, November 15, 2012
Rating:
No comments: