Snare wa East Coast awa producer wa filamu, tazama trailer ya movie aliyofanya – Shujaa
Kwa muda mrefu aliyekuwa member wa kundi la East Coast Team, ECT, rapper
Snare, amekuwa kimya na shughuli za muziki lakini ameamua kuelekeza
nguvu zake kwenye filamu.Kwa sasa Snare ni mtayarishaji wa filamu chini
ya kampuni iitwayo Afronode Film na December 1, 2012 anatarajia kuzindua
filamu iitwayo SHUJAA…
check out trailer yake hapa
Amani ni mmoja wa vijana aliyeguswa na kitendo cha Raisi JAKAYA MRISHO KIKWETE cha kuamua kupima VVU hadharani.Naye kuanzia hapo alijiwekea utaratibu wa kufanya hivyo kila baada ya miezi mitatu, na kwa bahati nzuri alikuja kufanya kazi katika shirika linaloshugulika na na kupima VVU na Ushauri nasaha.
Siku moja alikutana na binti mzuri Fransisca akiwa katika mazingira ya kujiuza (changudoa). Alimuona ni mzuri sana akampenda, na akataka kujua zaidi .Hadithi ya maisha ya yule msichana ndio yanamfanya amani awe na imani zaidi .Lakini jambo moja linatatiza kati yao je yule msichana ni salama? hakuna kinachoweza kufumbua fumbo hili zaidi ya kwenda kupima kitu ambacho Francisca hakuwa tayari kutokana na idadi ya wanaume aliotembea nao.
Ugumu wa jambo hilo haumkatishi tamaa amani, hatimaye anafanikiwa kuokoa maisha ya msichana huyo. Na kutimiza ndoto zake za kuwa shujaa kama Raisi Jakaya Kikwete.
Snare wa East Coast awa producer wa filamu, tazama trailer ya movie aliyofanya – Shujaa
Reviewed by Unknown
on
Monday, November 26, 2012
Rating:
No comments: