Top Ad unit 728 × 90

HAFLA YA UFUNGUZI WA KITUO CHA KOMPYUTA CHA KANISA ANGLIKANI PARISHI YA MAGUGU (MKOA WA MANYARA) DAYOSISI YA MLIMA KILIMANJARO TAREHE 6 JANUARI, 2013

Mwanafunzi Idrisa Hassan akimuonesha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi, viongozi na waumini wa kanisa Anglikani Magugu namna ya kutumia kompyuta wakati wa ufunguzi wa kituo cha kutolea elimu ya Komputa cha kanisa Anglikani Magugu, hafla ya ufunguzi ilifanyika kanisani hapo mapema jana.
Hafla hiyo ya ufunguzi ilitanguliwa na ibada takatifu iliyofanyika kanisani hapo magugu na baadaye kufuatiwa na maandamano yaliyoongozwa na viongozi wa kanisa ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi.
Katibu wa kanisa Anglikani parishi ya Magugu Bw.Dismas Charles akisoma taarifa fupi ya kituo cha kompyuta kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimb, uongozi wa kanisa na waumini wakati wa hafla ya kukifungua kituo hiko.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akifungua kituo cha kompyuta cha kanisa Anglikani Parishi ya Magugu (Mkoa wa Manyara) Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro jana.
Baadhi ya  wanafunzi wakiwa wanajifunza elimu ya komputa kwenye kituo cha kutolea elimu ya komputa cha kanisa Anglikana Magugu kilichofunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi mapema jana .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi kituo cha kompyuta cha kanisa Anglikani Parishi ya Magugu (Mkoa wa Manyara) Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro mapema jana.
HAFLA YA UFUNGUZI WA KITUO CHA KOMPYUTA CHA KANISA ANGLIKANI PARISHI YA MAGUGU (MKOA WA MANYARA) DAYOSISI YA MLIMA KILIMANJARO TAREHE 6 JANUARI, 2013 Reviewed by Unknown on Monday, January 07, 2013 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.