Top Ad unit 728 × 90

Ney kwenye BEEF na Bongo Movie!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, maarufu Ney wa Mitego, amejiingiza katika mtego wa mahusiano mabaya na wasanii wa kike wa filamu za Kitanzania (Bongo movie) kwa kile kilichodaiwa kuingiza shairi lenye maneno ya kashfa kwa wasanii hao.
Akiongea kwenye mahojiano na kituo kimoja cha television cha jijini Dar es salaam na kutakiwa athibitishe alichokiimba, Ney alithibitisha kuwa aliimba na kumaanisha alichokiimba, ndio ukweli wa tabia za wanawake walioingia katika tasnia hiyo na kuichafulia sifa za msanii wa filamu katika jamii.
“Nilichokiimba nina ushahidi nacho, kwa kuwa rafiki yangu alitokea kumpenda mmoja ya wasichana waigizaji, siku moja tukaenda klabu moja ya usiku, kwa bahati tukamuona, ndipo rafiki yangu akamkabili kumweleza upendo wake wa dhati, akajibiwa kwa kutanguliziwa swali kuwa, je, una fedha? hali iliyomduwaza,” alisema Ney.
Alibainisha kuwa rafiki yake alimkubalia na kumpa fedha yule msichana Sh 500,000, wakaondoka kwa kutumia gari la Ney na kuwaacha katika moja ya hoteli kubwa jijini ambapo walilala hapo.
Ney anadai siku iliyofuata walitafakari tabia ya mastaa hao wa filamu za Kitanzania, wakaafikiana na rafiki yake wafanye utafiti kama tabia hiyo ni ya yule binti tu au na wengine wapo hivyo.
Anasema usiku uliofuata walikutana na msichana mwingine maarufu ambaye rafiki yake alimkabili, akapata majibu kama ya yule wa awali akaenda naye hoteli kulala naye akapewa Sh 300,000.
Anasadikisha zoezi hilo lilienda kwa mara ya tatu kujiridhisha na utafiti wao, mara ya mwisho walimpata msichana maarufu ambaye yeye alitaka apewe dola 10,000 ambapo walipofanya mazungumzo alikubali kupokea Sh 600,000.
Ney akadai tangu hapo aliona wasichana wa filamu hizo ni wauza sura kwa ajili ya ukahaba, hali iliyomsukuma kuingiza shairi lisemalo makahaba waliokubuhu wapo ‘bongo movie’ na kuwa aliimba alichokishuhudia.
Msanii mmojawapo aliyehojiwa kuhusiana na tuhuma hizo za ngono zilizotolewa na Ney ni Shamsa a.k.a Ford, ambae alipinga vikali huku akidai Ney alitia mashairi hayo kutaka umaarufu na kuwashitua wapenda filamu za kibongo.
“Huyu msanii ameishiwa na ubunifu akaona atuchafue kupitia uimbaji, hakuna tabia kama hizo, anaropoka hana la kuimba, nashauri jamii impuuze,” alimalizia.
Ney kwenye BEEF na Bongo Movie! Reviewed by Unknown on Friday, August 31, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.