Top Ad unit 728 × 90

NIKKI MBISHI NA UMIKONI ALL STAR

Kuunga na kwa baadhi ya wasanii wakianza wa Kigoma all star ikifuatiwa na Morogoro All Star umeanza kuonekana ni mchezo ambao kwa baadae utawakera na kuwachosha baadhi ya watu hasa pale ambapo kila mkoa utataka kutengeneza  kollabo kama waliyoifanya wasanii kutoka mkoa wa kigoma.

Msanii Nikki Mbishi ameonekana kuliona hilo kwa mtazamo wa mbali kiasi cha kudiss katabia hako ambacho kametaka kuwaingia wasanii walio wengi ambao nao wameonekna kutaka kuiga umkoani all star kwa kusema katika ukurasa wake wa facebook kwamba "Tunakoendea kila msanii atatoa wimbo unaosifia mkoa wao Bongo bwana vya kufanya vimeisha" haya ni baadhi ya maneno ya Nikki Mbishi katika ukurasa wake wa facebook.

Hata Dj Mchomo analiunga mkono hili na hatusemei majungu ama nini kwani siku zote walikuwa wapi basi wafanye hivyo hata kwa kufanya show katika mikoa yao na ikiwa na lengo la kuchangia miradi mbalimbali au kutoa misaada kwa jamii hasa ukizingatia kwamba bado jamii yetu ina mambo mengi bado magumu... kwahiyo litakuwa ni suala la busara watu waw wanafanya show kama hizo ktk mikoa yao kwa kusudi ama lengo maalum la kimaendelea na sio kujionesha kwamba nani katoka wapi na nani mkali katika muziki.. na mbona kama hivo wapo wasanii wengi tu bado wanaikana mikoa yao na tunawajua walio wengi so kwa nini leo hii mjifanye kujionesha baada ya kuona wenzenu wamefanya kitu kama hicho?

Lingine ni kwamba wasanii hao hao hata wakifika katika mikoa yao ni watu ambao wanaongoza kwa kuwaringia mashabiki wao wa nyumbani ukizingatia wao ndio wa kujivunia kwa maana kwamba nakubalika nyumbani basi niwape ushirikiano lakini hao hao wasanii wakifika katika mikoa yao ndo wa kwanza kujificha na kutaka wasionekane sasa leo hii nawe unajifanya uanzishe 'umkoa wako all star ili iweje' kama vipi we potezea tu.........

Big Up sana Nikki Mbishi kwa kuliona hili!
NIKKI MBISHI NA UMIKONI ALL STAR Reviewed by Unknown on Wednesday, August 22, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.