Top Ad unit 728 × 90

‘BELLE 9′ APIGA COLLABO NA WASANII KUTOKA MAREKANI, ATAKA KUFIKA KIMATIFA ZAIDI…!!

WAKATI bongo ni wasanii wachache wanaofanya muziki unaolenga soko la kimataifa na kuvuka nje ya mipaka ya Afrika, nae kijana mdogo kutoa mkaoni Morogoro anayefanya vizuri kwenye soko Belly 9, amekiambia chanzo cha habari kuwa amefanya collabo na wasanii kutoka nchini Marekani ingawa nao bado ni chipukizi.

Mbali na wasanii hao wa Marekani pia Belly 9 alisema kuwa ameshafanya collabo nyingine na wasanii kama Nazizi kutoka Kenya na Cannibal huku akiamini kuwa kuvuka mipaka ya kufanya kazi na wasanii hao kunaweza kufungua njia nyingine ya kufika mbali zaidi.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na ngoma nyingine mpya inachokwenda kwa jina la  ‘Anayeishi naye’, ambayo ndani yake anapatikana kijana Ben Pol, wakati ngoma zake kama ‘Amerudi’, ‘Suma ya Penzi’, ‘Masogange’ bado zinafanya vizuri.

“Malengo yangu ni kutoka kimataifa kwani nafanya muziki ili nao uniweke kwenye nafasi fulani kimaisha, muziki ni ngumu pale unapoufanya kama mchezo lakini unakuwa mzuri pale unapoufanya kwa malengo na kujua ni kazi hivyo kwa upande wangu nalenga kufika mbali zaidi,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa hana mpango wowote wa kutoa albamu kwa mwaka huu, kwani tatizo kubwa linalomuumiza ni pale watu wanapotumia njia za mkato kama ku-burn albamu ya msanii huku wakisahau kuwa wao wanatumia gharamu nyingi za pesa na muda katika kutengeneza wimbo hadi unakuja kukamilika na kwenda sokoni.
‘BELLE 9′ APIGA COLLABO NA WASANII KUTOKA MAREKANI, ATAKA KUFIKA KIMATIFA ZAIDI…!! Reviewed by Unknown on Saturday, September 15, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.