Top Ad unit 728 × 90

Usaili wa video mpya ya DIAMOND!

Baada ya kurejea kutoka marekani kwenye ziara ya kimuziki iliyokuwa na mafanikio makubwa, msanii ambaye nyota yake kwasasa inashine kupita maelezo, Naseeb Abdul ‘Diamond’, anajiandaa kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao anategemea kuurelease soon.
Akiongea na darhotwire kwa njia ya simu, Peter Mwendapole toka kampuni la One Touch Solutions, watakaoratibu zoezi hilo amesema....“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu, ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.
DIAMOND AFAFANUA
Akijibu SMS ya mwandishi wetu iliyomtaka kueleza lengo la kufanya usaili huo , Diamond nia ni kuleta mapinduzi katika sekta ya muziki nchini, lakini pia kutengeneza ajira kwa ajili ya wasichana na wavulana, ambao wako mitaani lakini wanapenda muziki.
Usaili wa video mpya ya DIAMOND! Reviewed by Unknown on Saturday, September 15, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.