Top Ad unit 728 × 90

GARI LA MIZIGO LAPATA AJALI DODOMA

Gari kubwa la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajili T 574 AJA lililokuwa limebeba marobota ya pamba limpata ajali leo majira ya jioni katika Mzunguko wa Barabaraya Airport kuelekea Mailimbili na Bahi road maarufu kama Round about ya Posta lililokuwa katikati ya mzunguko huo.

Chanzo cha ajali hiyo kinasemekana ni mwendo wa gari hilo kuwa wa kasi na kuzidiwa na mzigo mkubwa uliokuwa juu ya gari hilo. Mpaka natoka eneo la ajali askari wa usalama barabarani pamoja na timu nzima ya uokoaji walikuwa wakijitahidi kuitoa mizigo hiyo na kuipakia katika gari lingine pamoja na kulinyanyua gari hilo ili kulitoa barabarani na hakuna mtu aliyeumia katika ajali hiyo.


GARI LA MIZIGO LAPATA AJALI DODOMA Reviewed by Unknown on Thursday, September 13, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.