Top Ad unit 728 × 90

DIAMOND: DAH! BINADAMU TUNATOKA MBALI SANA, HEBU TAZAMA HUKU NILIPOANZIA MUZIKI

 Daah! Maisha ni safari ndefu sana ndugu zangu na hakuna anae jua wapi anaelekea wala aliyezaliwa anajua chochote,siku zote mwanzo huwa mgumu sana ukiongeza na maneno ya watu ya kukukatisha tamaa basi ndio unazidi kuyaona Maisha magumu na kukata tamaa na kujiona huwezi kabisaaaa!... Mimi wakati naanza muziki nilikutana na mambo mengi sana ya kukatisha tamaa lakini siku zote sikuchoka kumuomba Mwenyezi Mungu anisaidie na kuzidisha juhudi kila dakika..... 
Naitumia nafasii hii pia kuongea na wasanii wachanga wanaochipukia kwenye sanaa ya muziki wasikate tamaa na hizi ni kama nguzo zinazoweza kukufanya angalau kupiga hatua.....Kwanza kabisa ni Maombi,Uvumilivu,Juhudi,Ubunifu na Heshima inahitajika sana.....Ukiangalia Video yangu ya Toka mwanzo na hiyo ya Mawazo niwazi kabisa utajionea utofauti mkubwa sana na utakubaliana na mimi ama kweli MAISHA NI SAFARI NDEFU SANA.  

hayo ni maneno ya Diamond ambayo aliyaandika katika mtandao wako wa 'Thisisdiamond'
DIAMOND: DAH! BINADAMU TUNATOKA MBALI SANA, HEBU TAZAMA HUKU NILIPOANZIA MUZIKI Reviewed by Unknown on Friday, October 19, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.